Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi msimu huu amekiongoza kikosi chake katika michezo 17 ya ligi kuu. Wananchi wameshinda michezo 14 na kutoka sare michezo mitatu tu hivyo kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama 45
Ni alama nane zaidi ya timu inayoshika nafasi ya pili, Simba huku timu zote zikiwa zimecheza mechi 17
Keshokutwa Jumamosi Yanga watacheza mchezo wao wa 18 pale watakapowakaribisha KMC kwenye mchezo ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Nabi ni kocha pekee aliyetwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi mara mbili msimu huu
Lakini kubwa zaidi, Nabi ameweka rekodi ya aina yake tangu alipotua Yanga mwanzoni mwa mwezi April 2021 akichukua nafasi ya Cedric Kaze ambaye baadae alirejeshwa kuwa Kocha Msaidizi
Tangu mwaka jana, Nabi amepoteza mchezo mmoja tu kwenye ligi kuu dhidi ya Azam Fc, April 23 mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Huo ulikuwa mchezo wake wa kwanza baada ya kusaini mkataba wa mwaka wa kuwaumikia Wananchi
Tangu wakati huo, Yanga imecheza mechi 23 za ligi kuu bila kupoteza mchezo
Nabi anafukuzia rekodi ya kucheza msimu mzima bila ya kupoteza mchezo