Hakuna mchezaji muhimu ataondoka - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Mar 2022
Hakuna mchezaji muhimu ataondoka - Hersi

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said ambaye ni Mjumbe Kamati ya ufundi klabu ya Yanga, amesema wako mbioni kuwaongeza mikataba wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu

Hersi amesisitiza kuwa Yanga haitawaachia nyota wake muhimu ambao wako katika mpango wa Kocha Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi

Msimu huu Yanga imedhamiria kutwaa ubingwa wa ligi kuu ili wapate nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao

Wananchi wanaongoza mbio za kuwania taji hilo pengine malengo hayo yanaweza kutimia ifikapo mwezi May 2022

Kikosi cha Nabi kimeshapata muunganiko, wakifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu wanaweza kufanya mambo makubwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao

Lakini kuna wachezaji kadhaa ambao mikataba yao inaelekea ukingoni, Hersi amewatoa wasiwasi Wananchi kuwa nyota hao wataendelea kubaki Jangwani

Mongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na nahodha Bakari Mwamnyeto, Farid Mussa, Zawadi Mauya, Yassin Mustafa, Kibwana Shomari, Deus Kaseke, Yacouba Sogne na mkongwe Saido Ntibazonkiza

"Tayari tulishaanza mazungumzo nao na wengine wanasubri kusaini mikataba tu. Tumekuwa na msimu mzuri mpaka sasa kutokana na ubora wa kikosi chetu. Hivyo hakuna mchezaji ambaye tutamuachia aondoke ," alisema Hersi

Kikosi cha Yanga msimu huu kimekuwa bora sana, mwishoni mwa msimu Wananchi watahitaji usajili wa maboresho tu katika nafasi chache

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’