Muda unakaribia kwenda kushuhudia burudani ya Wananchi katika uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC
Nyota na kinara wa mabao ligi kuu ya NBC Fiston Mayele ambaye amefunga mabao 10 na kutoa pasi za mabao matatu, atakuwa na nafasi nyingine ya kujiimarisha katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu
Mayele anachuana na Reliants Lusajo wa Namungo Fc ambaye pia ameweka kambani mabao 10 na kutoa pasi mbili za mabao wakati mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole anashika nafasi ya tatu akiwa amefunga mabao 8
Mayele ameweka rekodi ya aina yake mpaka sasa akifunga katika michezo minne mfululizo, amefunga jumla ya mabao matano katika michezo hiyo
Mechi saba zilizopita amepachika mabao sita kwenye ligi na kombe la FA
Kama atafunga leo utakuwa mchezo wa tano mfululizo Mcongomani huyo 'anatetema'