Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama klabu ya Yanga Simon Patrick amesema anaamini goli la kwanza la Yanga katika mchezo dhidi ya KMC hapo jana linastahili kupewa Mayele
Mayele aliunganisha mpira ulioparazwa na Denis Nkane, ulimgonga mlinzi Andrew Vicent wakati mpira huo ukielekea kimiani
Kumeibuka mjadala mkali kuhusu goli kama anastahili kupewa Mayele au ni goli la kujifunga Chikupe?
Haya hapa maoni ya Wakili msomi Simon;
"Sina mpango wa kuwakosea wale wote wenye mtazamo tofauti, lakini mpira wa miguu ni mchezo wa wazi na una misingi yake;
Narudia tena kusema, Goli la kwanza la Mayelle ni goli halali na wala sio Own Goal, kwanini?
Sheria za FIFA zimetoa “general definition” kwamba own goal ni mpira ulioingizwa kambani kwa kujifunga.
Kutokana na matukio kadhaa, Football Handbook ikaweka precedent guide inayotofautisha kati ya “Own Goal” na “Deflected Shot” na marefa wote ulimwenguni wanaufata huu muongozo kwenye maamuzi.
Pale ambapo Mchezaji anapiga shuti lisilokuwa na uelekeo wa golini halafu shuti likamgusa Mchezaji na kubadili uelekeo kwenda golini hiyo uhesabika “Own Goal” mfano ni yale magoli anajifunga Magwaya pale Man U
Mchezaji anapopiga shuti on target na ule mpira ukamgusa opponent bila kubadili uelekeo wa ulipokuwa unaelekea, hiyo uhesabika kama “Deflected Shot” na mpigaji hupewa goli lake.
Hivo basi, Shuti la Mayelle lilikua linaelekea golini kabisa, na hata Dante asingeugusa (kama kweli aliugusa) usingebadili mwelekeo hiyo inahesabiwa kama deflected shot na Mayelle lazima apewe goli lake"