Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto na Dickson Job ni miongoni mwa wachezaji 28 wanaounda kikosi cha timu ya Taifa kinachojiandaa na michezo ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya Afrika ya Kati (Machi 23) na Sudan (Machi 29)
Nyota sita wa Yanga wamejumuishwa katika kikosi hicho ambacho mwezi Juni kitaanza kampeni ya kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023
Wachezaji wengine ni Aboutwalib Mshery, Farid Mussa, Zawadi Mauya na Feisal Salum 'Fei Toto'
Wakiwa wachezaji wa kutegemewa kwenye safu ya ulinzi ya Yanga, Mwamnyeto na Job wanatarajiwa kuendeleza pacha yao katika timu ya Taifa
Kocha Kim Poulsen ameonyesha kuwa na imani nao kwani aliwatumia pamoja hata katika michuano ya kuwania tiketi ya kufuzu kombe la Dunia
Mwamnyeto na Job ndio pacha bora ya safu ya ulinzi katika ligi kuu ya NBC msimu huu
Ndani ya kikosi cha Yanga, ukuta wao umeruhusu mabao manne tu!