Baada ya kukamilisha tukio kubwa la kufunga ndoa, kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza ameanza mazoezi kujiweka sawa tayari kurejea kikosi mchezo ujao dhidi ya Azam Fc
Saido alipewa mapumziko ya wiki tatu baada ya kuumia kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, Saido alifunga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao yaliyofungwa na Fiston Mayele
Saido amekosa mechi mbili zilizopita kwenye ligi dhidi ya Geita Gold na KMC lakini kuanza kwake mazoezi ni ishara kuwa nyota huyo atajumishwa katika kikosi kitakachoikabili Azam Fc uwanja wa Azam Complex, April 06
Katika msimu huu Saido amefunga mabao sita na kutoa pasi za mabao matano na kumfanya kuwa mchezaji wa pili aliyehusika na mabao mengi zaidi katika kikosi cha Yanga baada ya Mayele
Saido amehusika katika jumla ya mabao 11 kwenye ligi wakati Mayele amehusika katika mabao 13, amefunga 10 na kutengeneza mabao matatu

