Ninja awashukuru viongozi Yanga, GSM kwa matibabu Tunisia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Mar 2022
Ninja awashukuru viongozi Yanga, GSM kwa matibabu Tunisia

Mlinzi wa Yanga Abdallah Shaibu 'Ninja' ameushukuru uongozi wa Yanga chini ya udhamini wa GSM kwa kufanikisha matibabu ya jeraha lake la goti nchini Tunisia

Ninja alisafirishwa kwenda kutibiwa Tunisia akiongozana na Kibwana Shomari, matibabu yao yakigharimiwa na GSM kwa asilimia 100

Katika mahojiano maalum na Yanga TV, Ninja amesema alianza kusumbuliwa na maumivu ya goti msimu uliopita baada ya mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0

"Baada ya mchezo ule niliendelea kusikia maumivu na wakati mwingine sikuyasikia, lakini kadiri nilivyokuwa nikifanya mazoezi maumivu yaliongezeka"

"Ilifika wakati nikawa sifurahii tena kucheza mpira na hata mazoezini nikawa sijitumi sana kutokana na maumivu niliyokuwa nikisikia"

"Baadae nikawaambia viongozi wangu juu ya tatizo lililokuwa likinisumbua ndipo wakati ambao mwenzangu Kibwana nae alipata majeraha sote tukapelekwa Tunisia kutibiwa"

"Nawashukuru sana viongozi na wadhamini GSM kwa kufanikisha matibabu yangu. Ilifika wakati nilifikiri nisingeweza tena kucheza mpira, walichofanya kina thamani kubwa kwangu"

"Siwezi kusema ni gharama kiasi gani imetumika lakini ni gharama kubwa sana. Baada ya matibabu nilitakiwa kukaa nje kwa wiki tatu, sasa nimetimiza wiki nne na nimeanza mazoezi mepesi"

"Natarajia baada ya wiki mbili nitakuwa nimepona kabisa tayari kurejea tena uwanjani," alisema Ninja

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’