Kikosi cha Yanga kinaingia kambini Avic Town leo kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa April 06 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Yanga inaingia kambini huku ikiwakosa nyota wake saba wanaokabiliwa na majukumu ya timu za Taifa
Walinda lango wawili Djigui Diarra na Aboutwalib Mshery wanaungana na Farid Mussa, Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job, Zawadi Mauya na Feisal Salum katika timu za Taifa
Yanga itaanza mazoezi jioni ya leo katika viwanja vya Avic Town
ADVERTISE HERE