Tanzania imetakata uwanja wa Benjamin Mkapa leo ikipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Afrika ya Kati katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki ambayo uko ndani ya kalenda ya FIFA
Tanzania ilifunga mabao yake kupitia kwa Novatus Dismas, Mbwana Samatta na George Mpole aliyeingia dakika za majeruhi na kufunga bao hilo
Vijana wa kocha Kim Poulsen walikuwa bora zaidi ya wapinzani wao, pengine walistahili ushindi mnono zaidi ya waliopata
Farid Mussa ameendelea kuitendea haki safu ya ulinzi upande wa kushoto Poulsen akimuingiza katika kipindi Cha pili na akatengeneza bao lililofungwa na Samatta
Tanzania itacheza mechi nyingine dhidi ya Sudan Machi 29 baada ya Botswana kufuta mchezo wao dhidi ya Tanzania uliokuwa upigwe Machi 26
ADVERTISE HERE