Upo uwezekano mkubwa msimu ujao Tanzania itatoa uwakilishi wa timu nne katika michuano ya CAF kama ilivyokuwa msimu huu
Yaani timu mbili zitashiriki ligi ya mabingwa na nyingine mbili zitashiriki kombe la Shirkisho barani Afrika
Mpaka sasa Yanga ina zaidi ya asilimia 70 kuwa itamaliza katika nafasi tatu za juu msimu huu na kujihakikishia kushiriki Kimataifa msimu ujao
Hata hivyo lengo kuu la Yanga ni kushinda ubingwa wa ligi kuu na kujihakikishia tiketi ya kushiriki ligi ya mabingwa
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi bado ana deni katika michuano ya Kimataifa hasa ikizingatiwa msimu huu timu ilitolewa raundi ya awali
Ujio wa wachezaji wengi wapya, muda mfupi wa maandalizi na kukosekana kwa vibali vya wachezaji Djuma Shabani, Khalid Aucho na Fiston Mayele yaweza kuwa sababu ambazo zilichangia Yanga ikashindwa kutamba msimu huu
Tayari Nabi amefanikiwa kupata muunganiko wa kikosi chake, akiwa pia anaendelea kuboresha maeneo yenye changamoto
Kwa jinsi Yanga 'ilivyoiva', msimu ujao Wananchi watakuwa na timu ya kuwapa raha kimataifa
Nabi amewahi kushinda kombe la Shirikisho (hili wanalocheza Simba) akiwa na klabu ya Leopards ya Congo
Hivyo ni kocha mwenye uzoefu wa michuano hii mikubwa barani Afrika