Takwimu zilizotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimebainisha kuwa kiungo wa Yanga Feisal Salum ndiye mchezaji aliyefanya kazi eneo kubwa la uwanja akikimbia wastani wa Kilomita 10.4 katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Afrika ya Kati
Katika mchezo huo kocha Kim Poulsen alimtumia Feisal kama kiungo huru aliyepanda timu iliposhambulia na kurudi kuzuia pale waliposhambuliwa 'Box-to-box'
Kwa sasa Feisal ni mmoja wa wachezaji tegemeo katika kikosi cha timu ya Taifa kutokana na umahiri wake uwanjani

ADVERTISE HERE