Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama wa klabu ya Yanga Simon Patrick ameteuliwa kuwa Wakili Msaidizi wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC)
Simon amesema ni furaha kwake kupata nafasi hiyo ya kuwa Wakili wa Mahakama ya Kimatifa
"Nimefurahi sana kuteuliwa kuwa mmoja wa Mawakili Wasaidizi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Nitatumia uwezo wangu wote kuisaidia mahakama hii kwenye kutenda haki"
"Nafarijika zaidi kuwa Mtanzania wa kwanza kupewa fursa hii adhimu na ya kipekee, nitahakikisha utendaji wangu unafungua fursa kwa Wanasheria wenzangu wengine waTanzania kwani najua uwezo tunao," amesema Simon
Simon amesema uteuzi huo hautaathiri majukumu yake mengine

ADVERTISE HERE