Kiungo fundi wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto' anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili baada ya kupata majeraha akiwa katika timu ya Taifa
Juzi Daktari wa timu ya Taifa alitoa taarifa juu ya aina ya majeraha yanayomkabili Feisal, akipendekeza nyota huyo kupata muda mrefu wa kupumzika ili kutibu changamoto hiyo
Feisal amebainisha pia alipata majeraha ya goti kwenye mazoezi ya Stars, majeraha hayo yatamlazimu kukaa nje ya uwanja kwa angalau wiki mbili
Feisal amesema baada ya kucheza mechi na Afrika ya Kati alimaliza vizuri ila waliporejea mazoezini ndio alipata maumivu ya goti
"Nitakuwa nje ya uwanja kwa muda usiopungua wiki mbili baada ya kupata maumivu ya goti, nipo nyumbani Zanzibar naendelea na matibabu, naamini baada ya muda huo nitakuwa sawa," alisema Feisal
Feisal atakosekana katika michezo miwili inayofuata dhidi ya Azam Fc (ligi kuu) na Geita Gold (ASFC)