Unaambiwa Yanga imepania kwelikweli kupata ushindi dhidi ya Azam Fc katika mchezo utakaozikutanisha timu hizo ambapo utapigwa Jumatano, April 06 kwenye uwanja wa Azam Complex
Ni hivi; Yanga inaweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa msimu huu kama itashinda mchezo huo na mchezo utakaofuata dhidi ya Simba ambao utapigwa April 30
Huu ni mchezo ambao wachezaji wanautaka kwelikweli hasa kutokana na mazingira yaliyopo
Wachezaji wana dhamira ya kutwaa ubingwa lakini piaย kucheza michezo 18 pasipo kupoteza, imewatengenezea maaduni wengi ambao wanasubiri wafungwe ili wapate la kuzungumza
Yanga ilirejea kambini juzi Ijumaa chini ya kocha mkuu Nasreddine Nabi kuiandaa dozi ya Azam Fc
Ni mwendo wa mazoezi makali huko Avic Town, hao Azam Fc wajiandae kisaikolojia kwani hawatatoka salama hapo kwenye uwanja wao wa Azam Complex