Makambo anaamini atafunga Ligi Kuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Apr 2022
Makambo anaamini atafunga Ligi Kuu

Mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo amesema anaamini muda wake wa kufunga mabao katika ligi kuu ya NBC umekaribia

Makambo bado hajafanikiwa kuzifumania nyavu kwenye ligi msimu huu licha ya kuwa amefunga mabao matatu katika michuano ya kombe la FA na kufunga mabao kadhaa katika michezo ya kirafiki

Moja ya changamoto zinazomkabili msimu huu ni kutopata muda mrefu wa kucheza katika kikosi cha kwanza mbele ya Fiston Mayele ambaye amekuwa na msimu bora zaidi

"Jambo muhimu kwangu ni kuisaidia timu kupata matokeo bila ya kujali kama nimefunga au la, nitaendelea kupambana kila ninapopewa nafasi, naamini nitafunga katika michezo inayokuja," alisema Makambo

Katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mafunzo Fc uliopigwa uwanja wa Azam Complex hivi karibuni, Makambo alifunga moja ya mabao ya Yanga katika ushindi wa mabao 3-2

Katika mchezo huo kocha msaidizi wa Yanga Cedric Kaze alisema Makambo alionyesha kiwango bora na huenda akapata nafasi zaidi kwenye kikosi cha kwanza katika mechi zilizobaki

Kaze alisema kwenye mchezo huo walijaribu kutumia washambuliaji wawili (4-4-2) ambapo Mayele na Makambo walicheza pamoja katika dakika 30 za mwisho

Alisema kutokana na ugumu wa michezo iliyobaki kumaliza msimu, zipo baadhi ya mechi watalazimika kutumia washambuliaji wawili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’