Azam Fc vs Yanga, ni fainali nyingine kwa Wananchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Apr 2022
Azam Fc vs Yanga, ni fainali nyingine kwa Wananchi

Keshokutwa Jumatano Yanga itashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuikabili Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC mzunguuko wa 19

Utakuwa mchezo wa nne tangu kuanza kwa duru ya pili Yanga ikifanikiwa kushinda michezo yote mitatu ya kwanza katika duru ya pili

Hii inaitwa dabi ya Mzizima kwani ukiacha mchezo dhidi ya Simba, mchezo wa pili kwa ukubwa hapa Tanzania ni mchezo unaozikutanisha Yanga na Azam Fc

Yanga imejichimbia kambini Avic Town tangu Ijumaa iliyopita ikijiandaa na mchezo huo ambao Wananchi wanazihitaji alama zote tatu

Ni msimu ambao Yanga inahitaji kutwaa ubingwa baada ya kuukosa kwa misimu minne mfululizo ukichukuliwa na watani zao Simba

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi katika moja ya mahojiano yake, alisema pamoja na kuongoza ligi kwa tofauti ya alama 11 dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili, wataanza kufikiria ubingwa kama watashinda michezo miwili ya ligi katika mwezi huu

Mchezo wa kwanza ni huu dhidi ya Azam Fc na mchezo wa pili ni dhidi ya Simba ambao utapigwa April 30

Nabi anafahamu kama atapata ushindi katika michezo hii ni wazi atakuwa amejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’