Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema Jumatano ni siku muhimu kwa mashabiki wa timu hiyo akiwaasa kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Azam Complex kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc
Manara amesema hawaidharau Azam Fc wakitambua ni moja ya timu bora msimu huu, wakiwa wanacheza katika uwanja wao wa nyumbani
Lakini amesema Yanga msimu huu imejiwekea malengo na wamejipanga kuhakikisha wanayatimiza
"Wananchi naendelea kuwakaribisha katika Show kubwa Jumatano hii, mje mkijidai ingawa hatuwezi kuwadharau Azam Fc ukizingatia wapo kwao Chamazi"
"Lakini sisi ndio bingwa wa muda wote wa Taifa hili na tuna jambo letu msimu huu. InshaAllah tutapata matokeo mazuri Jumatano hii," alisema Manara
Yanga ndio vinara wa ligi kuu ya NBC wakijikusanyia alama 48 baada ya kushuka dimbani mara 18
Ni uongozi wa tofauti ya alama 11 dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 37
Ushindi dhidi ya Azam Fc utawafanya Wananchi wazidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa idadi ya alama nyingi (14)