Himid Mao
Kutokana na klabu ya Yanga kukumbwa na tatizo 'sugu' la kiungo mkabaji, mashabiki wengi na hata baadhi ya viongozi wamekuwa wakitamani klabu impate nahodha wa Stars kwa wachezaji wa ndani Himid Mao 'Mkami'.
Mao yuko vizuri kwenye nafasi hiyo, juzi tu amelidhihirisha hilo kwenye michuano ya Cosafa nchini Afrika Kusini.
Anao uwezo wa kucheza nafasi zote za kiungo iwe chini au juu. Na kingine kizuri zaidi Mao ni mahiri sana katika ukabaji, ana nguvu, ana pumzi yani ni jembe kwenye sekta hiyo.

Himid Mao Mkami
Najua jitihada zilifanyika kupata sahihi ya huyu mbabe, lakini tatizo ni mkataba wake unaomalizika Novemba 2017.
Azam hawako tayari kwa majadiliano ya aina yoyote zaidi ya kutaka 'mpunga mrefu' mezani ili wamuachie licha ya kuwa amebakisha miezi minne tu mkataba wake umalizike.
Kwa kuwa imebaki chini ya miezi sita kwenye mkataba wake, Mao anaruhusiwa ufanya mazungumzo na hata kusaini mkataba wa awali(pre-contract agreement) na klabu yoyote.
Hivyo upo uwezekano Yanga ikamsajili halafu ikaanza kumtumia mwezi Novemba, je mwenyewe yuko tayari?
Erasto Nyoni
Erasto Nyoni ametimiza miaka 29 mwezi Mei. Huyu ni kiraka na anaweza kucheza nafasi zote za ulinzi na kiungo.
Habari njema ni kwamba mkataba wake na Azam FC umemalizika mwezi huu wa saba.
Ukizungumzia wachezaji viraka huyu ndiye sasa. Unaweza kumfananisha na Mbuyu Twitte ambaye aliondoka Yanga kwenye mzunguuko wa pili wa VPL msimu uliopita.

Nyoni akimkaba mshambuliaji wa Ivory Coast Gervinho
Nyoni amekuwa kwenye kiwango cha juu kwa muda mrefu. Nyoni amedumu kwenye kikosi cha Stars kwa miaka 11 kwani aliitwa kwa mara ya kwanza na kocha Maximo mwaka 2006.
Majuzi tumemshuhudia kocha wa Taifa Stars akimtumia kwenye nafasi ya kiungo mkabaji na aliimudu vyema nafasi hiyo.
Kuumia kwake kwenye mchezo dhidi ya Zambia kuliwapa wepesi Zambia kupata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Stars kwenye mchezo wa nusu fainali michuano ya Cosafa.
Habari njema huyu nae ni miongoni mwa wanaoangaliwa na uongozi na huenda akasajiliwa kwa kuwa hata kocha Lwandamina anamkubali sana.
Nyoni hana kikwazo kutoka Azam FC kwa kuwa mkataba wake wa kuitumikia klabu hiyo umemalizika na bado hajasaini mkataba mpya.
FERNANDO BONGNYANG
Huyu ni Mcameroon ambaye anafanyiwa majaribio lakini bado hajasajiliwa, kocha anataka kujiridhisha na uwezo wake kwanza.
Tangu jana anaonekana kwenye kikosi cha Yanga lakini ifahamike bado hajasajiliwa.

Bongnyang Fernando wa katikati
Huyu ni kiungo mkabaji, ni nahodha wa kikosi cha Cameroon kwa wachezaji wa ndani. Ana umri wa miaka 29 na ametokea Cotton Sports ya huko Cameroon.
Huyu uchezaji wake hautofautiani sana na Vicent Bossou. Ingawa yuko polepole lakini ni makini sana. Pasi zake ni za uhakika pia ana uwezo mkubwa wa kukaba.
Ni jambo jema kwa kocha Lwandamina kutaka ajiridhishe kabla ya kumuongeza kikosini isije ikawa kama kwa Justine Zulu 'Mkata Umeme'.
Je lile kombora la maangamizi lililoahidiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya usajili linawahusu hawa?
Jumapili sio mbali, wanajangwani vuteni subira, msimu ujao kuna vilabu vitaomba 'poo' nawaambia.

ADVERTISE HERE