Msemaji wa Yanga Haji Manara amesisitiza kuwa msimu huu hawana sababu ya kukosa ubingwa wa ligi kuu kutokana na ubora wa timu waliyonayo
Manara amesema sio kwamba wanazungumza porojo, wamejipanga na wamedhihirisha dhamira ya kutwaa ubingwa katika michezo 19 iliyopita
Wananchi wako kileleni mwa msimamo wa ligi wakijikusanyia alama 51 baada ya michezo hiyo 19
Ni alama 11 zaidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili. Manara amesema haoni Yanga inawezaje kukosa ubingwa msimu huu na kwa hakika kama wataukosa yuko tayari kuhama nchi
"Yanga imekaa miaka minne bila ya ubingwa, Wanachama na Mashabiki hawawezi kusubiri. Na ndio maana mimi nikisikia vichekesho na mamb ya kikatuni wanavyosema ooh Yanga imezoea kuongoza ligi lakini baadae Simba anachukua ubingwa, haya ni maisha ya kukariri, kama tutakosa ubingwa msimu huu mimi nahama nchi!," alitamba Manara