Mchezaji kiraka katika kikosi cha Yanga Yannick Bangala yuko tayari kurejea kikosini baada ya kupona majeraha
Bangala aliukosa mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc, kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi akimuweka miongoni mwa wachezaji wa akiba
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema Bangala anaweza kurejea dimbani kuikabili Geita Gold katika mchezo wa robo fainali kombe la FA hapo kesho
Aidha Kaze amethibitisha kuwa viungo Feisal Salum 'Fei Toto' na Khalid Aucho wataukosa mchezo huo pamoja na Salum Abubakar 'Sure Boy' mwenye kadi tatu za njano
Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kesho ikiwa na dhamira moja tu, kupata ushindi dhidi ya Geita Gold na kutinga nusu fainali kombe la FA
ADVERTISE HERE