Yanga vs Geita Gold Fc leo, robo fainali FA Cup

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Apr 2022
Yanga vs Geita Gold Fc leo, robo fainali FA Cup

Majira ya saa moja usiku leo, Wananchi watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Geita Gold ukiwa ni mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)

Huu ni mchezo wa tatu kuzikutanisha Yanga na Geita Gold zikiwa tayari zimecheza mechi mbili za ligi kuu Yanga ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi zote

Leo wanakutana katika mchezo wa mtoano ambao lazima mshindi apatikane pale uwanja wa Benjamin Mkapa

Ni mchezo unaotarajia kuwa na upinzani mkali kwani Geita Gold ni moja ya timu imara kwenye ligi hasa baada ya maboresho waliyofanya katika usajili wa dirisha dogo

Mchezo huu unawakutanisha vinara wa kupachika mabao katika ligi kuu, Fiston Mayele akiongoza na mabao yake 11 huku George Mpole wa Geita Gold akiwa amefunga mabao tisa

Baada ya ushindi dhidi ya Azam Fc katika mchezo uliopita kwenye ligi, Yanga imepania kuendeleza ubabe wake kwa kushinda dhidi ya Geita Gold leo

Ushindi utawahakikishia kutinga nusu fainali na pengine watakutana na watani zao Simba ambao watacheza na Pamba Fc katika mchezo ambao haujapangiwa tarehe

Hata hivyo hautakuwa mchezo mwepesi, Geita Gold wanaonolewa na Fred Felix Minziro, wamedhihirisha kuwa timu imara na Wananchi watahitaji kuwa katika ubora wao ili kupata ushindi leo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’