Baada ya kufanikiwa kutinga nusu fainali kombe la FA kwa ushindi wa mikwaju ya penati dhidi ya Geita Gold juzi, kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi aliwapa wachezaji mapumziko ya siku mbili
Jumatano Yanga inarejea mazoezini kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu unaofuata dhidi ya Simba ambao utapigwa April 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wamedhamiria kushinda mchezo huo ili kuongeza tofauti ya pointi dhidi ya Simba kuwa 13
"Timu itarejea mazoezini Jumatano kuanza maandalizi ya mchezo wa dabi. Kwetu huu ni mchezo muhimu kwani tunahitaji kushinda ili kuongeza tofauti ya alama dhidi ya anayetufuatia kuwa 13"
"Benchi la ufundi watatupatia program yao ya maandalizi ili kuhakikisha wanapata kila watakachohitaji ili kuona tunakuwa na maandalizi mazuri," alisema Bumbuli
Yanga itakuwa na takribani wiki tatu za kujiandaa na mchezo huo ambao unaweza kuisogeza Yanga karibu na ubingwa wa 28