Yeyote aje nusu fainali FA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Apr 2022
Yeyote aje nusu fainali FA

Baada ya kutinga nusu fainali ya kombe la FA, Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wako tayari kwa mchezo utakaofuata kwenye hatua ya nusu fainali bila ya kujali watakutana na nani

Juzi Yanga ililazimika kusubiri mikwaju ya penati kutinga nusu fainali dhidi ya Geita Gold baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za mchezo uliokuwa na ushindani mkali

Yanga ina nafasi kubwa ya kukutana na watani zao Simba kwenye mchezo wa nusu fainali, Simba itacheza na Pamba Fc mchezo wa robo fainali ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumzia mchezo dhidi ya Geita Gold, Kaze amesema ushindani waliokutana nao katika mchezo huo waliutarajia

"Geita walicheza vizuri, walipata muda wa kutosha wa kujiandaa, lakini sisi tuliingia na uchovu baada ya mchezo wetu dhidi ya Azam Fc siku tatu zilizopita. Walikuwa vizuri kuzuia wakipata mpira walikuwa na kasi ya kushambulia, mechi ilivyokuwa ikiendelea ndivyo walivyozidi kujiamini"

"Tumeona hata kwenye michezo miwili ya ligi tuliyokutana na Geita ni timu nzuri, tumeifunga lakini imetupa tabu sana naamini kama itaendelea kuwa hivi itaendelea kufanya vizuri kwenye michezo yake iliyobaki"

"Tumejiwekea malengo ya kushinda taji la FA, tumeingia nusu fainali na tuko tayari kukutana na timu yoyote katika hatua hiyo," alisema Kaze

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’