Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema umoja na ushirikiano kutoka kwa wadhamini, viongozi, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki ndio siri ya kufanya vizuri msimu huu
Nabi jana alikuwa miongoni mwa wadau waliohudhuria futari iliyoandaliwa na GSM ambapo alisema Wanayanga wanapaswa kuendelea kuwa wamoja ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao mwishoni mwa msimu
"Watu wengi wamenipongeza kutokana na mwenendo mzuri wa timu yetu msimu huu lakini sikufanya kazi peke yangu. Ni kwa sababu kila mmoja kuanzia kwa wadhamini mpaka mashabiki wametimiza wajibu wao katika kuiunga mkono timu yao. Tunapaswa kuendelea hivi mpaka mwisho mwa msimu"
"Bado hatujatwaa ubingwa, tuna mechi nyingi kukamilisha msimu huu lakini jambo muhimu kwetu ni kuhakikisha tunaendelea kupata matokeo katika kila mchezo ili tuweze kujikusanyia alama nyingi zaidi kuliko wengine," alisema Nabi
Nabi amesema wameanza maandalizi kujiandaa na mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa April 23 katika uwanja wa Benjamin Mkapa