Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto amekuwa na kiwango bora msimu huu haishangazi kuona tetesi zimeanza kumuhusisha na klabu nyingine
Mkataba wa Mwamnyeto unamalizika mwishoni mwa msimu lakini tayari Yanga kupitia wadhamini wao GSM wameanza mchakato wa kuhuisha mkataba wake
Hivi karibuni Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Yanga alisema suala la usajili wameliacha mikononi mwa kocha Nasreddine Nabi na kuwa wanasubiri mapendekezo yake
Hata hivyo Hersi amesema hawataruhusu mchezaji yeyote ambaye yuko katika mipango ya kocha kuondoka akiwa huru

ADVERTISE HERE