Bodi Ligi Kuu Tanzania(TPLB) imebadili uwanja wa mchezo wa Ligi kuu ya NBC kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Yanga SC
Mchezo huo awali ulipangwa kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa lakini sasa mchezo huo utachezwa mnamo Mei 4, 2022 saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika uliopo mkoani Kigoma
Sababu ya mabadiliko hayo ni timu mwenyeji (Ruvu Shooting FC) kutumia nafasi ya kikanuni ya kucheza mechi mbili katika uwanja mwingine kwa michezo ya nyumbani miongoni mwa viwanja visivyokuwa na michezo ya Ligi Kuu [Kanuni ya 9(7)]
ADVERTISE HERE