Hawa Namungo Fc wana deni la Mayele

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Apr 2022
Hawa Namungo Fc wana deni la Mayele

Hivi karibuni, Bodi ya Ligi ilirudisha nyuma mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Namungo Fc ambao sasa utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa April 23 2022

Huu ni mchezo mwingine muhimu kwa Yanga kuibuka na ushindi ili kuendelea kuukaribia ubingwa wa ligi kuu ya NBC

Baada ya kuambulia alama moja mkoani Lindi, Wananchi wamepania kuzibakisha alama zote tatu Dar

Katika moja ya mahojiano yake, mshambuliaji wa Yanga kinara wa mabao Fiston Mayele aliitaja Namungo Fc kama miongoni mwa timu ambazo ana deni nazo

Namungo ni moja ya timu ambazo Mayele hajazifunga kwenye ligi, nyingine ni Simba, Mbeya City, Ruvu Shooting, Polisi Tanzania na Tanzania Prisons

"Mwezi huu nina deni ya timu mbili, Simba Sc na Namungo Fc nawasubiri kwa hamu uwanja wa Mkapa," alisema Mayele

Mayele anaongoza mbio za kuwania ufungaji bora akiwa amefunga mabao 11 na kutoa pasi tatu za mabao

Baada ya mchezo dhidi ya Namungo Fc, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Simba, April 30 dimba la Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’