Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema wamejipanga kufanya vizuri katika michuano ya Kimataifa msimu ujao na watadhihirisha hilo katika usajili wa nyota wapya wanaokusudia kuwasajili
Yanga ambayo iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 51, imedhamiria kutwaa ubingwa wa ligi kuu ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Manara alisema wametenga dola Mil 1 kwa ajili ya usajili wa wachezaji wapya ambao idadi yao haitazidi watano
"Kwa mujibu wa kanuni za CAF, Yanga itaanzia raundi ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa (wakitwaa ubingwa wa ligi kuu) na Simba wataanzia hatua ya awali labda washinde taji la Shirikisho. Nawaahidi, Yanga itakuwa klabu ya kwanza kushinda taji la Afrika"
"Msimu huu tutafanya pre-season ambayo haijawahi kufanywa na klabu yoyote hapa Tanzania na tutafanya usajili ambao haujawahi kutokea, thamani ya wachezaji tutakaowasajili ambao watakuwa wanne au watano ni zaidi ya dola Mil 1 (Tsh Bil 2.4)," alitamba Manara