Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ametimiza mwaka mmoja tangu alipojiunga na mabingwa hao wa kihistoria April 20 2021
Katika mwaka wake mmoja, Nabi ameishi katika ahadi alizozitoa kwa kuifanya Yanga kuwa timu imara yenye kushindania mataji
Tangu atue Yanga, Nabi amepoteza mchezo mmoja tu wa ligi kuu akiiongoza Yanga msimu huu kucheza mechi 19 pasipo kupoteza mchezo
Tangu msimu uliopita, Yanga imecheza jumla ya michezo 26 pasipo kupoteza
Kikosi chake kimekaa kileleni mwa msimamo wa ligi na alama 51, matumaini ya kutwaa ubingwa yakiwa ni makubwa
Malengo yake ya msimu huu ni kuiongoza Yanga kutwaa taji la FA na ligi kuu, kwenye FA Yanga iko hatua ya nusu fainali
Yanga ina malengo makubwa zaidi msimu ujao hasa kwenye michuano ya Kimataifa, msimu huu Nabi hakupata matokeo mazuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa akitolewa katika hatua ya awali
Hata hivyo zipo sababu za msingi ambazo zilichangia Yanga isifanye vizuri katika michuano hiyo na hivyo kumuondoa lawamani Nabi