Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Boniface Ambani amesema kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga msimu huu Fiston Mayele, bado ana kazi ya kuthibitisha ubora wake kwa kufunga mabao zaidi katika michezo iliyobaki
Mayele amefunga mabao 11 katika michezo 19, akisalia na michezo 11 katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu
Ambani alikuwa mfungaji bora wa ligi kuu msimu wa 2008/09 akifunga mabao 18 katika michezo 22
Mshambuliaji huyo raia wa Kenya amesema anafurahia kazi anayoifanya Mayele msimu huu lakini anatamani kumuona akifunga mabao mengi zaidi ili kuvunja rekodi walizoweka wao
"Nadhani amefunga zaidi ya bao kumi saizi lakini tuko mzunguko wa pili kwa hiyo anahitaji kuboresha wastani wake wa kupachika mabao. Wakati mimi nacheza Yanga timu zilikuwa 12 pekeyake sasa zipo 18 kwa hiyo yeye mwenyewe kama Straika lazima aangalie takwimu zake asifunge bao moja tu akafurahi," alisema Ambani
Kama ataweza kufunga katika kila mchezo miongoni mwa mechi 11 zilizosalia, Mayele ataivunja rekodi hiyo ya Ambani kwani atafikisha mabao 20
Mayele amejiwekea malengo ya kutwaa tuzo ya ufungaji bora msimu huu