Leo Jumapili ya April 24 mchezo wa pili wa dabi ya kinadada kati ya Yanga Princess dhidi ya Simba Queens utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Huu utakuwa kama mchezo wa utangulizi kabla ya kaka zao Yanga na Simba kukutana katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa April 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga Princess imepepesuka kidogo msimu huu wakishika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Wanawake, hata hivyo huu utakuwa mchezo wa kisasi
Yanga Princess ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 na Simba Queens katika mchezo wa duru ya kwanza
Katika mchezo uliopita kwenye ligi kuu ya Wanawake, Princess waliichapa JKT Queens mabao 2-0
ADVERTISE HERE