Tutawatumia Namungo Fc kutuma salamu Simba - Bumbuli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Apr 2022
Tutawatumia Namungo Fc kutuma salamu Simba - Bumbuli

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wanafahamu Namungo Fc wanaocheza nao kesho mchezo wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, ni moja ya zile timu zilizotajwa kuwavurugia Wananchi kutwaa ubingwa msimu huu

Bumbuli amesema Yanga imejipanga kushinda mchezo huo na watawatumia Namungo Fc kuwapelekea ujumbe Simba kuwa zamu yao imefika!

"Hawa Namungo Fc ni miongoni mwa zile timu ambazo zilitajwa kupewa kazi ya kutuzuia tusichukue ubingwa. Tumeshapiga wengine wote, wamebaki hawa (Namungo Fc) halafu watakaofuata ni hao kaka zao wanaowatuma"

"Tumejipanga kupata ushindi dhidi yao ili sasa wakawapelekee ujumbe kaka zao wawaambie kuwa kazi waliyowatuma imewashinda na sasa ni zamu yao wenyewe," alitamba Bumbuli

Mapema leo akihojiwa na chombo kimoja cha habari, kocha msaidizi wa Namungo Fc, Jamhuri Kiwhelo 'Julio' alitamba kuwa wanakuja jijini Dar es salaam kuifunga Yanga

Julio alisema Simba bado ina nafasi ya kutetea ubingwa kwani anajua Yanga watapoteza mchezo dhidi yao (Namungo) na kisha kupoteza mchezo dhidi ya Simba April 30

"Simba anaweza kutetea taji msimu huu, kitu ambacho pia kimesaidia kwa Yanga msimu huu hakuna viporo lakini Yanga wanaongeza jitihada za kushinda"

"Sasa hivi Yanga wamewazidi Simba alama 10 lakini ninachojua ni kuwa tunacheza na Yanga kesho, tunataka tuvunje mwiko wa Yanga kufungwa, tukiwafunga kutakuwa gape la alama saba, wakicheza na Simba wenyewe zinabaki alama nne"

"Alama nne unawezakutana na Mbeya City ukapata pancha ukaja ukakutana na mwingine ukapoteza, utapata wapi huo ubingwa?," alisema Julio

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’