Saido, Yacouba kuikosa Namungo Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Apr 2022
Saido, Yacouba kuikosa Namungo Fc

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wanapata ushindi muhimu dhidi ya Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Akizungumza katika mkutano na Wanahabari mapema leo, Kaze alisema nyota wote wa Yanga wako tayari isipokuwa Saido Ntibazonkiza na Yacouba Songne ambao ni majeruhi

Kaze amewapa Wananchi habari njema juu ya kurejea kwa Feisal Salum, Khalid Aucho na Chico Ushindi ambao wako tayari kwa mchezo huo

"Tunaamini utakuwa mchezo mgumu kwani tunacheza na timu nzuri ambayo iko nafasi ya tatu kwenye ligi. Tumejipanga kwani tunajua umuhimu wa alama tatu za mchezo wa kesho"

"Maandalizi yetu yamekuwa vizuri, tumepata nafuu kwenye wachezaji walikuwa kwenye majeraha kuna waliorudi, Feisal amerudi, Khalid Aucho na Chico Ushindi wote wamerudi kufanya mazoezi na wenzao"

"Wachezaji wote wako vizuri wanafahamu umuhimu wa mchezo huo. Kitu kikubwa ni kucheza kitimu na kupambania jezi ya Yanga ili kupata matokeo"

"Kuna wachezaji ambao tutawakosa, Saido ambaye hajapona sawasawa majeraha yake na Yacouba ambaye amekuwa nje kwa muda mrefu," alisema Kaze

Kaze ameongeza kuwa mchezo wa kesho utakuwa tofauti na vile walivyocheza mchezo wa duru ya kwanza ambao walilazimishwa sare ya bao 1-1

"Mchezo wa kesho utakuwa tofauti, mchezo wa duru ya kwanza ulikuwa wa tano, wachezaji hawakuwa wamezoeana sawasawa na sasa tumeshacheza mechi nyingi na muhimu zaidi tunacheza katika uwanja wa nyumbani. Namungo Fc nao ni wazuri ni moja ya timu zinazocheza soka la nguvu na mahiri sana katika mashambulizi ya kushitukiza, tutahakikisha tunawadhibiti "

Kaze amesema kukosekana kwa kocha Nasreddine Nabi haliwezi kuwa tatizo kwani hata yeye ni kocha mzoefu wa ligi ya Tanzania na kama kocha amefanya kazi muda mrefu hivyo hakutakuwa na tatizo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’