Licha ya klabu ya Yanga kukata rufaa kupinga kadi nyekundu aliyopewa kocha Nasreddine Nabi kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Geita Gold, Kamati ya Mashindano imetupilia mbali rufaa hivyo Nabi atatumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu na kulipa faini ya Tsh 500,000/-
Aidha, kulingana na taarifa iliyotolewa na TFF leoe, Kelvin Yondani wa Geita Gold amefungiwa michezo mitatu pamoja na kulipa faini ya Tsh Milioni moja baada ya kumkanyaga kwa makusudi Fiston Mayele katika mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kufuzu nusu fainali kwa ushindi wa mikwaju ya penati

ADVERTISE HERE