Kikosi cha Yanga kimeshawasili jijini Mbeya kwa usafiri wa ndege kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho 'FA' dhidi ya Ihefu Fc.
Mechi hiyo inachezwa leo kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya.
Viongozi wa matawi na baadhi ya mashabiki wa Yanga wa jijini Mbeya ndio waliyoilaki timu wakati ikiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA).
Baada ya kuwasili viongozi hao wameiongoza timu hiyo kuelekea Hoteli ya Ifisi iliyoko nje kidogo ya Jiji la Mbeya ambako wameweka kambi kwa muda.
Meneja wa Yanga Hafidhi Saleh amesema wachezaji wote walioko kwenye msafara huo wapo salama.
Mchezo dhidi ya Ihefu utapigwa saa kumi jioni na utarushwa mubashara na kituo cha runinga cha Azam kupitia chaneli ya Azam Sport 2.

ADVERTISE HERE