Waacheni washangilie, ndio ubingwa wao huo

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
1 May 2022
Waacheni washangilie, ndio ubingwa wao huo

Wakati mwingine inachekesha sana unapoona mashabiki wa timu inayojinasibu kuwa kubwa zaidi nchini wanashangilia eti mchezaji fulani hajawafunga!

Na wakati huohuo ni hao hao waliokuwa wakimbeza mchezaji huyo kuwa hawamuhofii kwa kuwa hana madhara

Ndio! ushindi wa mashabiki wengi wa Simba pale uwanja wa Benjamin Mkapa jana ni kuona Fiston Kalala Mayele hajafunga mbele ya mlinzi wao Hennock Inonga Baka

Sherehe hii inathibitisha ni kwa kiasi gani walikuwa wakimuhofia sana Mayele kutokana na makali yake katika kufunga

Lakini mashabiki hao pia wamesahau nao uwanjani walikuwa na mshambuliaji wao Christ Mugalu ambaye alishindwa kufurukuta mbele ya walinzi wa Yanga Dickson Job na Bakari Mwamnyeto

Kabla ya mchezo , mashabiki wa Simba walijinasibu kuwa wana wachezaji hatari kama Bernard Morrison, Clatous Chama, Pape Ousmane Sakho na hata Kibu Denis

Lakini baada ya dakika 90 hakuna aliyezungumza kilichowatokea wachezaji hao mbele ya bwana mdogo Kibwana Shomari

Kelele zilikuwa nyingi zaidi kuhusu Chama lakini shughuli aliyokutana nayo mbele ya kina Aucho na Bangala katika dakika 45 za kwanza, Pablo hakumrejesha uwanjani kwenye kipindi cha pili

Huyu Morrison mpaka akachoma bisibisi mshabiki wa Yanga baada ya mchezo, hasira za kushindwa kufurukuta mbele ya Kibwana!

Simba tayari wamefahamu hawana chao kwenye ligi msimu huu hivyo wanajaribu kujifariji kupitia kwa Mayele

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’