Vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga leo wana nafasi ya kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kama wataibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting
Ni mchezo wa raundi ya 22 ambao utapigwa uwanja Lake Tanganyika, mkoani Kigoma
Baada ya watani zao Simba kuvutwa shati mkoani Lindi hapo jana kwa kulazimishwa matokeo ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Namungo Fc, Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 12
Ushindi leo utawafanya waongeze 'gap' kufikia alama 15 na kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa
Yanga inahitaji kushinda michezo mitano kati ya tisa iliyobaki ili kutwaa ubingwa
Hesabu hizo wanaweza kuzianza leo mbele ya Ruvu Shooting kule Kigoma
Hata hivyo hautakuwa mchezo mwepesi kwani Ruvu Shooting nao wanahitaji matokeo ili kujiondoa katika hatari ya kuteremka daraja
Katika mchezo wa duru ya kwanza timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1