Mchezo wa ligi kuu kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, umemalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Ruvu walikuwa imara katika kujilinda licha ya majaribio kadhaa ambayo Yanga walifanya
Wananchi ni kama walikosa bahati kwani majaribio mawili ya Fiston Mayele katika kipindi cha kwanza yaliishia kwenye mwamba
Ni matokeo ambayo sio mabaya sana kwa Yanga kwani Wananchi wanaendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 56
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Tanzania Prisons, utapigwa May 09 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE