Licha ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Ruvu Shooting hapo jana, kiungo wa Yanga Khalid Aucho amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa wamejipanga kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu
Aucho alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshuka uwanja wa Lake Tanganyika hapo jana katika mchezo huo ambao Yanga haikuwa katika ubora uliozoeleka kutokana na hali ya uwanja kutoruhusu soka la pasi fupifupi
Aucho amesema sio matokeo waliyoyahitaji lakini hayataathiri mpango wao wa kutwaa ubingwa msimu huu
"Tunawashukuru mashabiki wetu kwa kuendelea kutuunga mkono. Najua sio matokeo tuliyoyahitaji siku ya leo (jana) lakini tunawaahidi kuwa tutaendelea kupambana kuhakikisha tunatwaa ubingwa msimu huu," alisema Aucho
Yanga inatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam leo kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumatatu May 09