Afisa Mhamasishaji wa Yanga Haji Manara amesema hawana haja ya kujiweka katika presha baada ya kulazimishwa suluhu dhidi ya Ruvu Shooting kwani mkakati wao wa kutwaa ubingwa msimu huu bado uko salama
Hata hivyo Manara amesema bado Yanga haijatwaa ubingwa kwa kuwa alama walizonazo sasa zinaweza kufikiwa na timu nyingine, wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha wanapambana katika kila mchezo ili kukusanya alama nyingi ambazo hazitaweza kufikiwa na timu nyingine
Manara amesema ltakuwa jambo la aibu wao kukosa ubingwa na kama jambo hilo litatokea pasi wanastahili kuchapwa viboko!
"Kila siku narudia na kurudia tena na tena, Yanga bado hatujashinda Championship ya Msimu huu, Points zetu Kwa sasa bado kuna Team zinaweza kuzifikia"
"Tusibweteke hata kidogo. Lakini pia Tusijipe Presha ya jani la Mpera eti lolote linaweza kutokea , Tutakuwa Wapuuzi zaidi ya Wapuuzi kukosa ubingwa huu, na tutastahiki viboko wote"
"Tuendelee kupambana hadi tone la mwisho Kwa kujua ubingwa upo mikononi mwetu na tumuombe Mungu wetu malengo yetu yatimie Insha'Allah," alisema Manara