Wakati mwingine ni vyema kukubali na kujipanga upya pale unaposhindwa huo ndio uungwana
Siku ya jana Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally alitoa kauli ya kuponda ligi ya msimu huu kuwa ni dhaifu eti kwa kuwa timu nyingi zinapambana kujiepusha na kushuka daraja
Naamini kauli hii ameitoa baada ya kuona klabu yake ya Simba ina nafasi ndogo ya kutwaa ubingwa lakini kama ingetuwa tofauti tusingesikia kauli ya aina hiyo
Ukweli ni kuwa msimu huu timu zote zimejipanga, hasa kutokana na kitita cha fedha kilichowekwa na Azam Media
Msimu huu bingwa wa Ligi Kuu atapata Sh 500 milioni, wa pili Sh250 milioni, watatu Sh225 milioni, wa nne Sh 200 milioni.
Timu itakayomaliza ya tano itapata Sh 65 milioni, 60 milioni timu itakayomaliza ya sita na ya saba itapata 55 milioni, na bonusi hiyo itaendelea kushuka hadi kwenye timu itakayocheza Playoff ambayo itapata bonusi ya Sh 20 milioni
Kila mwa mwezi timu zinapata karibu Tsh Milioni 40 kutoka Azam Media na fedha nyingine kutoka kwa Wadhamini wakuu NBC na wengine
Timu 14 kuwa katika hatari ya kushuka daraja sio udhaifu, bali ni ishara kuwa ligi imekuwa na ushindani, timu zote zinakaribiana uwezo
Ukiondoa Yanga na Simba ambazo zina ushindani wao, kwa timu nyingine 14 ushindani umekuwa mkubwa
Msimu huu timu zinalipa mishahara, zinasafiri na kufika katika vituo vyao kwa wakati huwezi kulinganisha na misimu ya nyuma ambayo wachezaji walikuwa hawalipwi na wakati mwingine kushindwa kusafiri kwa wakati vituoni
Kama ni udhaifu wa ligi basi ilikuwa nyakati hizo ambazo timu zilikuwa na hali duni ya kiuchumi lakini si sasa, wakati ambao kila timu inaweza kukidhi mahitaji yake