Himid Mao anaweza kutua Yanga

Admin By Admin
•
15 Jun 2017
Himid Mao anaweza kutua Yanga
Kiungo wa timu ya Azam FC, Himid Mao, amesema yupo mbioni kuvunja mkataba na klabu yake hiyo ili kukamilisha mipango yake ya kwenda kucheza soka la kulipwa.

Mao anatajwa kuwa katika mikakati ya kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, lakini aligoma kuweka wazi ukweli wa jambo hilo.

Hivi karibuni Mao alidai mkataba wake na Azam utamalizika Novemba mwaka huu, lakini mipango ya sasa ambayo wamejiwekea na wakala wake ni kucheza soka nje ya nchi.

Alisema wakala wake tayari ameanza mazungumzo na Azam ili wavunje mkataba na pia anapambana kufanikisha mikakati ya kumtafutia maisha mengine ya soka nje ya nchi.

“Nitaondoka Azam lakini sitasajiliwa Tanzania, mkataba wangu na Azam unatarajia kumalizika Novemba mwaka huu na sasa tumeanza mazungumzo ya kuuvunja.

“Nataka niondoke kama mchezaji huru ili nitakaposajiliwa na klabu nyingine nisifungamane na upande wowote,” alisema Mao.

Aidha, Mao aliongeza kuwa hakuna timu yoyote hapa nchini ambayo imefanya naye mazungumzo, huku akisisitiza kwamba hayupo tayari kufanya hivyo kwani anaangalia mbali zaidi kulingana na mipango yake.

Alisema bado ataendelea kuonekana na kikosi cha Azam hadi mipango yake itakapokaa sawa pamoja na mkataba wake kuvunjwa.

Kama kiungo huyo ataondoka, kikosi cha Azam kitazidi kubomoka kwani tayari kimeondokewa na wachezaji wake mahiri waliotamba msimu uliopita, John Bocco, Aishi Manula na Shomari Kapombe ambao wote wametua Simba.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →