Matchday; Yanga vs Tanzania Prisons, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 May 2022
Matchday; Yanga vs Tanzania Prisons, NBC PL

Vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga leo wanaendelea na msako wa ubingwa wa 28 pale watakaposhuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Tanzania Prisons ukiwa ni mchezo wa ligi kuu raundi ya 23

Baada ya Wananchi kukosa ushindi katika michezo miwili iliyopita, huu ni mchezo ambao vijana wa kocha Nasreddine Nabi wataingia dimbani wakiwa na dhamira ya kuondoka na alama zote tatu

Hata hivyo wanakutana na Tanzania Prisons ambayo nayo inapambana kujiondoa katika nafasi za hatari ya kuteremka daraja

Katika michezo nane iliyobaki, kama Yanga itaweza kushinda michezo mitano, basi itajihakikishia kutwaa ubingwa mapema

Hivyo ni mchezo ambao Wananchi wanazihitaji alama zote tatu ili kuendelea kusogea karibu na ubingwa

Leo benchi la ufundi litaongozwa na kocha Nabi mwenyewe baada ya kumaliza adhabu ya kadi nyekundu

Nabi atakuwa na kikosi chake kamili, ni mchezaji mmoja tu Yacouba Songne ambaye bado hayuko tayari kucheza mechi za ushindani

Mchezo utapigwa kuanzia saa moja usiku

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
42m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’