Wananchi leo hawahitaji kitu kingine zaidi ya ushindi dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi jana aliweka bayana utayari wa kikosi chake kuelekea mchezo huo ambao utapigwa kuanzia saa moja usiku
Bila shaka Nabi atarejesha kikosi chake cha ushindi baada ya mabadiliko yaliyofanywa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting ambao ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto leo anatarajiwa kurejea kikosini baada ya kupumzishwa katika mchezo uliopita akitarajiwa kuanza sambamba na Dickson Job
Djuma Shabani nae hakuanza mchezo uliopita, leo bila shaka atarejea katika nafasi yake upande wa kulia huku Kibwana Shomari akitarajiwa kurudi upande wa kushoto
Yannick Bangala na Khalid Aucho bila shaka wataanza pamoja katika eneo la kiungo wakati Saido Ntibazonkiza, Feisal Salum na Jesus Moloko wakitarajiwa kushirikiana na Fiston Mayele katika eneo la ushambuliaji
Huu ni mchezo ambao Yanga inahitaji ushindi, Nabi lazima ashushe silaha zake zote za maangamizi