Alama moja waliyoipata Yanga jana kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Prisons, imewahakikishia kukata tiketi ya kushiriki michuano nya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao
Yanga imefikisha alama 57 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote kuanzia nafasi ya tatu
Msimu ujao Tanzania itatoa timu mbili kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, ni Simba pekee ambayo inaweza kufikisha alama 57
Hesabu ya Yanga sasa ni kusaka alama 14 kati ya 21 zilizosalia ili kujihakikishia ubingwa wa ligi kuu msimu huu

ADVERTISE HERE