Fiston Mayele kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga anapitia wakati mgumu baada ya kucheza dakika 270 pasipo kufunga
Kabla ya mchezo dhidi ya Simba, Mayele alitoka kufunga katika mechi saba mfululizo
Hali kama hii humtokea mchezaji yeyote, jambo muhimu, anahitaji kusaidiwa kisaikolojia ili kuhakikisha anarejesha makali yake
Ni wazi umahiri wake unawakera wengi hasa kutokana na umaarufu aliopata kwa staili yake ya KUTETEMA
Wapo walioanzisha kampeni chafu zenye lengo la kumshusha chini wakiamini pia kwa kufanya hivyo watakuwa wameiathiri Yanga pia
Utaona ni kwa kiasi gani hata wachezaji wenzake wanatamani kumuona Mayele anafunga ili kumrejeshea hali ya kujiamini
Naamini Mayele atarejesha makali yake kwenye michezo inayofuata, muhimu asaidiwe, pia mashabiki hawapaswi kumuongezea presha
Lakini pia Yanga ina wazee kina Mpili nao wafanye kazi yao! Waswahili wenye nia ovu hawashindwi kutumia silaha aina yoyote ili kuhakikisha HATETEMI