Kikosi cha Yanga leo kimeanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa Jumapili, May 15 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi asubuhi aliwapeleka vijana wake Gym kuweka miili yao sawa baada ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons
Jioni Yanga inatarajiwa kuendelea na mazoezi ya kawaida Avic Town tayari kwa mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, mchezo ambao Yanga inazihitaji alama zote tatu





ADVERTISE HERE