Yanga imerejea kutoka mkoani Dodoma ambako jana waliweza kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji
Ni ushindi ambao umeiweka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 11 dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili
Yanga imefikisha alama 60 baada ya kucheza mechi 24 wakati Simba ina alama 49 baada ya kucheza mechi 23
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Mbeya Kwanza, Jumamosi, May 21 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea mkoani Mara kuifuata Biashara United tayari kwa mchezo utakaopigwa May 24
Alama sita za mechi hizi mbili zinaweza kuiweka Yanga katika nafasi bora zaidi ya kutangaza ubingwa kwani kimahesabu watakuwa wamesalia na alama tano tu wamalize kazi
Hata hivyo kama watani zao Simba watakosa ushindi katika michezo yao inayofuata, Yanga inaweza kutangaza ubingwa mapema zaidi
Simba itacheza na Azam Fc May 18 kule Chamazi kisha kuelekea Mwanza kuifuata Geita Gold, May 21 halafu watacheza na KMC May 25 jijini Dar es salaam
Simba inaweza kufikisha alama 70 kama itashinda michezo yake saba iliyobaki, Yanga imebakisha alama 10 tu kufikisha alama 70
Sare au kipigo chochote kwa Simba kitairahisishia kazi Yanga kutangaza ubingwa