Juni 30 ndio tarehe ya mwisho ambayo CAF itapokea majina ya timu zitakazoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho msimu ujao
Ndio maana TFF imelazimika kusogeza nyuma Ratiba ya mechi za nusu fainali kombe la FA, ambazo zitapigwa mwishoni mwa mwezi huu
Yanga tayari imekata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa, viongozi wanapaswa kuhakikisha wanakamilisha michakato yote ya usajili mapema ili kuepuka changamoto zilizojitokeza msimu huu
Bila shaka viongozi wa Yanga wamejifunza na yaliyotokea mwanzoni mwa msimu ambapo Yanga ilishindwa kuwatumia wachezaji muhimu kama Khalid Aucho, Djuma Shaban na Fiston Mayele baada ya ITC zao kuchelewa
Mashabiki wana matumaini makubwa kuwa timu yao itafanya vizuri kwenye michuano ya msimu ujao, uongozi unapaswa kuhakikisha kila mchezaji hasa nyota wapya watakaosajiliwa wanakuwa na sifa ya kushiriki michuano hiyo
Katika misimu michache iliyopita, imezoeleka katika kila michuano ya Kimataifa utasikia mchezaji fulani anakosekana kwa sababu ITC yake imechelewa
Bila shaka jambo hilo halitarajiwi kujitokeza katika michuano ijayo