Jana nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto alisaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Yanga
Mwamnyeto anakuwa mchezaji wa pili kuongezewa mkataba mwezi huu baada ya Kibwana Shomari
Inafahamika kulikuwa na jitihada kutoka upande wa pili kuwashawishi wachezaji hao waweze kuwasajili
Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said aliwahi kusema kuwa hakuna mchezaji ambaye Kocha Nasreddine Nabi atamuhitaji katika mipango yake ataondoka
Kauli hiyo imedhihiri baada ya kuwapa mikataba mipya nyota hao
"Wananchi wametaka mimi ni nani nikatae?," ni kauli ya Mwamnyeto baada ya kusaini mkataba mpya
Msemaji wa Yanga Haji Manara ameweka msisitizo kuwa kwa mazingira ya sasa hakuna mchezaji anayeweza kutoka Yanga kwenda kujiunga na timu nyingine na pia hakuna mchezaji ambaye watamtaka atagoma kusajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria